Header

Nick Mutuma afurahishwa na haya kutoka kwa Vanessa Mdee kwenye MTV Shuga

Muigizaji wa muda mrefu aliyepata umaarufu zaidi katika moja ya mchezo wa maigizo mkubwa Afrika “MTV Shuga” kutoka nchini Kenya ‘Nick Mutuma’ aliyecheza kama ‘Leo’ katika msimu huu mpya wa MTV Shuga ameelezea uzoefu alioupata katika kufanya kazi na msanii maarufu kutoka Tanzania The real Cash Madame a.k.a Vanessa Mdee.

Vanessa Mdee

Akizungumza na Dizzim Online Nick Mutuma amesifia mengi aliyokutana nayo katika msimu huo mpya ambapo ameelezea kila kilichomfurahisha katika kushiriki na Vanessa na kutaja alichokiona kwake. Alimtaja Vanessa kama msanii na muigizaji aliyeonekana kuwa na kipaji cha aina yake mbali kuwa hakuwa na uzoefu wa kuwa katika tasnia hiyo ya maigizo.

“nimekuwa muigizaji ambaye nimeshiriki kwenye vipindi vyote vya msimu na imekuwa ni furaha kubwa sana kwangu kufanya kazi na waigizaji wakubwa barani Afrika na watu mwenye uzuji wa hali ya juu zaidi katika tasinia hii ya maigizo…msimu huu umefanyika Afrika Kusini na umekuwa msimu mkubwa na mzuri kwangu na kilichonifurahisha zaidi ni matukio yote ya msimu yatakayoifanya Shuga iwe ndefu na tamu zaidi…kikubwa zaidi nilijisikia vizuri kushiriki katika mzimu huu na mmoja kati ya marafiki zangu wa karibu na msanii kutoka Afrika Mashariki ‘Vanessa’…ilikuwa ni furaha kipindi chote cha msimu kwasababu anajua anachokifanya na yuko makini linapokuja suala la maana…alikuwa ni mtu wa kutaka kujua zaidi ili aweze kufanya kitu kizuri zaidi inagwa kutokuwa na uzoefu zaidi ilikuwa ni changamoto kwake” Alisema Nick Mutuma.

Baadhi ya washiriki wa kiume wa msimu mpya wa MTV Shuga msimu mpya

Akizungumzia vipande vilivyo mtoa kijasho muigizaji Nick Mtuma amesema kuwa ameogeza ujuzi zaidi kupitia MTV Shuga mbali na kuwa katika tasnia hiyo kwa muda mrefu lakini iliweza kuwa rahisi katika vipande vingi kwasababu aliweza kufanya kazi na watu wenye uzoefu na ujuzi wa hali ya juu na waliowaongoza katika kufanikisha vitu vizuri. Akizungumzia  upande wa Vanessa amesema vipo vipande mbalimbali ambavyo vilikuwa changamoto hasa kati yake Vanessa na Emmanuel ambavyo vitaongeza utamu zaidi na kumpongeza kwa kufanya vizuri katika msimuu mpya wa Shuga.“kwa upande wa Vanessa vipo vipande ambavyo vilimuwia vigumu na kumpa changamoto hasa ambavyo alishiriki kati yake na Emmnuel ambavyo mtaviona but i think she killed it at the end of the day” Aliongeza Nick Mutuma.

 

Comments

comments

You may also like ...