Header

Azam FC wakubali yaishe waanza mandalizi ya Msimu ujao

Mabingwa wa Kombe la Mapinduzi wenye makazi yao nje kidogo na Dar es saalam, Azam FC baada ya kusuasua msimu huu Ligi Kuu Tanzania Bara, wameweka bayana kuanza taratibu mikakati ya usaji wa nguvu, hususani safu ya ushambuliaji katika msimu ujao.

Akizungumza na gazeti la Dimba Kocha wa Azam, Aristica Cioaba, amesema kwamba wakati wanaelekea kufikia ukingoni mwa ligi, hivi sasa wanaendelea kuangalia wachezaji ambao wanaweza kuwa msaada mkubwa kwenye kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao

“Hutuwezi kuweka wazi sana usajili wetu, lakini hilo ni jambo muhimu ambalo tunaendelea kulifanyia kazi wakati tunaelekea mwishoni mwa ligi na wakati huo huo tukitarajia kuanza msimu mpya, hivyo usajili ni suala nyeti,” alisema kocha huyo.

Azam FC ni moja ya timu zilizokuwa zinapewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa msimu huu, lakini ilipepesuka katika baadhi ya mechi, hasa zile zilizofanyika uwanja wao wa Chamazi Complex.

Comments

comments

You may also like ...