Header

Facebook wakiri makosa juu ya muuaji wa facebook

Makamu wa rais wa shughuli za kimataifa za Facebook Justin Osofsky

Baada ya tukio la mauaji ya mzee Robert Godwin mwenye umri wa miaka 74 kwa kupigwa risasi na Steve Stephens huku akiweka tukio hilo live katika mtandao wa facebook ambaye alijiua katika harakati kabla kutiwa mbaloni kwa kujipiga risasi, wahusika wa mtandao wakiri kuwa kwenye makosa kufuatia tukio hilo.

Muuaji Steve Stephens

Makamu wa rais wa shughuli za kimataifa wa mtandao huo bwana Justin Osofsky amekiri kitengo cha kuondoa jumbe, picha za video mtandani zisizofaa kushindwa kutimiza jukumu la kuondoa picha za Steve alizokuwa mara tu wakati akienezea taarifa za dhumuni la kufanya mauaji, video ya muaji na video mubashara ilioonesha muaji hata akitubu kuingia mtandao na kukaa kwa muda usiopungua masaa 2.

Katika posti ya blog ya makamu huyo wa rais wa shughuli za kimataifa alisema “tunajua kuwa tuhahitaji kufanya vizuri”

kufuatia ufanisi wa kuvizuia na kuondoa vitu hatarishi katika mtandao.

Osofksy aliweka pamoja na kalenda ya matukio yalioingia mtandaoni.

Nakala ya ratiba kama ilivyoripotiwa na BuzzFeed:

11:09 PT – Video ya kwanza ya dhamira ya kuua ilipakiwa na hakuripotiwa kwa Facebook.

11:11 – Video ya pili ya upigaji wa risasi kupakiwa.

11:22 – Mtuhumiwa anakiri kufanya mauaji nakuonyesha kwa kutumia Facebook Live, ambayo ilionyesha kwa muda wa dakika 5.

11:27 – Live video ilifiska mwisho na kutolewa taarifa muda mfupi baadaye.

12:59 – Video ya kupigwa kwa risasi ilitolewa taarifa ya kwanza.

1:22 p.m. — Akaunti ya mtuhumiwa aliondolewa na video zote hazikuweza kupatikana kwenda kwa watumaji wa mtandao.

Kulingana na kalenda ya matukio, kulikuwa na nafasi kubwa kati ya wakati video ya upigaji risasi kuripotiwa na wakati wa kuondolewa na kampuni.

“lilikuwa ni ukio la kiharifu la kutisha sana — mambo kama hayo hayana nafasi katika mtandao wa facebook, na nikinyume cha sheria na sera zatu ambazo tunasimamia”  Osofsky aliandika katika blog. kama matokeo ya mfuatano wa tukio hilo,amaesema wanapitia na kukagua mtiririko wao wa taarifa ili kuwa na uhakika wa watu wanaoweza kuripoti video na vitu vingine ambavyo vinakiuka viwango vyetu kwa urahisi na kwa haraka iwezekanavyo.

kampuni yao inatarajia kubadilisha jinsi watumiaji wanavyoweza kuripoti maudhui na wataongeza ufanisi wa kampuni katika uwezo wa kuondoa taarifa zisizofaa kwa haraka.

Comments

comments

You may also like ...