Header

Gerald Pique achukizwa na ushindi wa Real Madrid

Beki wa kati wa FC Barcelona, Gerard Pique hajafurahiswa kabisa na kitendo cha Real Madrid kuwaadhibu Bayern Munich goli 4-2 jana usiku kwenye michuano ya Klabu bingwa barani Ulaya (eufa Champions League) hasa kitendo cha muamuzi wa mchezo huo kutoa kadi nyekundu kwa kiungo wa Bayern Arturo Vidal.
Kati kati ya mchezo Pique alirekodi video fupi kwenye ukurasa wake wa facebook akiangalia mtanange huo huku akitikisa kichwa na kisha kufuta muda mfupi baadae akiashiria kuwa Madrid walibebwa kwa Vidal kupewa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu Marco Asensio wa Madrid na kutolewa nje katika mechi ya pili ya robo fainali kati ya Madrid na Bayern waliokuwa wageni.
Bayern ilipoteza mechi hiyo kwa kufungwa mabao 4-2. Pique ameonyesha hisia zake na kusema kosa hilo la mwamuzi, ndiyo limeibeba Madrid,Hata hivyo, ameonekana kueleza hisia zake kwa kitaalamu akitumia alama ya desh tu alizoweka kwenye ukurasa wake wa Twitter baada ya kufuta posti yake Facebook.
https://twitter.com/3gerardpique/status/854438221564063747
Madrid na Barcelona ni wapinzani wakubwa nchini Hispania na Leo Barcelona wana kazi kubwa ya kuing’oa Juventus ambayo katika mechi ya kwanza ilishinda kwa magoli 3-0.

Comments

comments

You may also like ...