Header

Jiandae kwa kolabo ya Rayavnny na Rapa kutoka Kenya Khaligraph Jones

Msanii wa muziki wa kiazazi kipya kutoka Tanzania Rayvanny anayezidi kufanya vizuri na wimbo wake ‘Nikumbushe’ alioshirikiana na muimbaji wa muziki wa njili kutoka nchini Kenya ‘Bahati’ azungumzia taarifa na ukweli wa kushirikiana na Rapa kutoka nchini Kenya Khaligraph Jones.

Akizungumza na Dizzim Online kutoka mjini Stockholm nchini Sweden ‘Rayvanny’ amethibitisha kukamilika kwa audio na video ya kolabo yao na Khaligraph na kinachosubiriwa ni muda muafaka na makubaliano ya pamoja ili kazi itoke rasmi iliyoonesha kuwa kuna kila dalili za kazi hiyo kuja kuwa kubwa kulingana na uwezo wa wasanii hawa kukutana katika wimbo wa pamoja.

“yeah ni kweli project yetu imeisha…i mean project yangu mimi na Khaligraph, tushafanya audio, tushafanya video so tunasubiri tu time na makubaliano yetu yakae sawa tuweze kutoa ngoma” Alisema Rayvanny.

Hata hivyo Rayvanny kwasasa yuko katika furaha kubwa ya kuitwa baba ambapo hakusita kuzungumzia furaha yake.

“kiukweli namshukur sana mungu kwa kunipa zawadi ya mtoto, naona kabisa kama maombi yangu yamejibiwa, pia mtoto ni baraka ujue kutoka kwa Mungu na nampenda sana mwanagu and i love my baby too” Alimalizia Rayvanny.

Rapa Khaligraph Jones

Rapa Khaligraph Jones kwasasa anafanya vizuri na ngoma yake ‘Micasa Sucasa’ aliyomshrikisha mpenzi wake ambaye pia ni rapa ‘Cashy’ anatazamiwa kuigia nchini Tanzania kwa lengo la kuachia wimbo wae aliomshirkisha Rayvanny pia kutambulisha nyimbo zake nyingine.

 

Comments

comments

You may also like ...