Header

Madee aisaliti Arsenal kwenye michuano ya Klabu bingwa barani Ulaya #UEFAChampionsLeague

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva kutoka Tip Top Connection Madee ameweka wazi ushabiki wake kwa Ronaldo ukilinganisha na wachezaji wengine ambao wanakipiga kunako bara la Ulaya huku akim’mwagia sifa kem kem mshambuliaji huyo wa Real Madrid.

Madee amesema utofauti wa Ronaldo na wachezaji wengine  ni kwamba anaweka rekodi kila kukicha na ni mchezaji ambae anaonesha uwepo wake kwenye mechi kubwa na zile muhimu pale ambapo klabu yake inahitaji ushindi.

Uchezaji wa Ronaldo na Messi ni vitu viwili tofauti,lakini kwa mapenzi naona Ronaldo ni bora zaidi ya Messi na sio kwa messi ila kwa kila mchezaji ukiniuliza swali hilo,Ronaldo amecheza karibia timu 3 kubwa mbili kwenye timu tofauti tofauti ukilinganisha na Messi ambae hajapata changamoto yoyote kwani yupo pale pale Barcelona“Amesema Madee kwenye mahojiano yake na Dizzim Online.

Madee aliulizwa pia ni Timu gani anayoishabikia kwenye michuano ya klabu bingwa barani ulaya ( EUFA ) kwa msimu huu baada ya timu yake Dam Dam ya Arsenal kutolewa Madee alisema  “Ukiniambia timu ninayoishabikia mimi ni Arsenal lakini kwenye UEFA timu ambazo zilizobakia mimi naishabikia Real Madrid ni timu ambayo napenda rangi ya jezi yao,Napenda morale wao wanapokuwa wametanguliwa na jinsi wanavyopambana kupata matokeo pia nampenda sana Zidane”

Klabu ya Real Madrid imefuzu hatua ya Nusu Fainali ya Klabu bingwa jana usiku baada ya Ronaldo kupiga Hatrick dhidi ya Bayern Munich kwenye ushindi wa goli 4-2 .

 

Comments

comments

You may also like ...