Header

Mohammed Fakhi awavua nguo Viongozi wa Simba

Mchezaji wa Klabu ya Kagera Sugar Mohammed Fakhi amekuwa Gumzo kufuatia sakata la kucheza akiwa na  kadi 3 za Njano lilopelekea  Simba kupewa pointi 3 za mezani hatimae akiri kupigiwa simu na viongozi wa Simba.

Fakhi amesema amekuwa akipigiwa Simu na Baadhi ya Viongozi wa Simba wakimtaka Aseme Ukweli kwenye kamati ya sheria, katiba na hadhi za wachezaji kwamba ni kweli alicheza akiwa na kadi 3 za njano.Lakini Mchezaji huyo amesema yeye ameshasema Ukweli kuwa hakuwa na kadi 3 za Njano kama Viongozi hao wa Simba walivyotaka aseme kuhusu utata wa suala hilo.
Nimepigiwa simu ndiyo na watu wa Simba wakitaka nipindishe maneno kuhusu kadi 3 za njano ila ukweli Mimi nimeeleza ukweli wote“Alisema Fakhi kwenye mahojiano yake na EFM.

Comments

comments

You may also like ...