Header

Pancho Latino atoa sababu za kutosikika kwenye muziki

Mtayarishaji wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania  mwenye sifa za kipekee kwenye kutengeneza muziki wa bongo fleva Pancho Latino ametaja sababu ya kutosikika kwenye muziki wa bongo fleva kwasasa.

Akizungumza na Dizzim Online Pancho, amesema “suala la mimi kutokusikika kila wakati nafikiri ni decision niliyoamua toka mwaka juzi baada ya wasanii wengi kuondoka hapa kwenye lebo yangu, niliamua kutokufanya kazi na wasanii tofauti tofauti kwa sababu mwisho wa siku nikagungua natumika bila kujijua kiasi kwamba mtu anakuja studio mnarekodi vizuri mnapatana nyimbo ikitoka baada ya show atatakuletea kiasi kadhaa lakini hafanyi hivyo, anakuja mara ya pili anakuongopea the same lies au tofauti unakuja kugundua producer hauna maendeleo msanii ana maendeleo, kwa hiyo nilivyogundua hicho kitu nikaona kwamba sasa kama nikifanya kazi sipati chochote na nisipofanya sipati chochote ni bora ni  focus na kitu kimoja nachokipenda mimi kwamba moyo wangu utaridhika hata kama nitafanya nisilipwe nitafanya kwa moyo mmoja na nitakuwa happy kuliko kuwa unhappy kwa kufanya kazi ya msanii ambapo roho inaniuma”
Hata hivyo Pancho ameongeza kuwa aliamua kutokufanya kazi kwasababu ya roho mbaya ya baadhi ya wasanii ambao hawapendi mtayarishaji aendelee na hawako tayari kulipa bei stahiki ya huduma ya kutayarisha,na kuhaidi mapinduzi na kuendeleza misingi ya kuendelea kuweka muziki mzuri katika muziki wa Tanzania.

Comments

comments

You may also like ...