Header

Xabi Alonso na Philipp Lahm waukimbia usiku wa Klabu Bingwa Barani Ulaya

Baada ya jana Bayern Munich kutupwa nje kwenye michuano ya Klabu Bingwa Barani Ulaya  kwa kuchapwa magoli 4-2 dhidi ya Real Madrid kiungo Xabi Alonso pamoja na nahodha wa Beyarn Munich Philipp Lahm ilikuwa ni michezo yao ya mwisho kwenye michuano hiyo.

Alonso pamoja Lahm wote wametangaza kustafu kucheza soka mwisho mwa msimu huu kitu ambacho kinawafanya jana kuwa ndio ulikuwa mchezo wao wa mwisho wa michuano ya Ulaya

Kwenye michuano ya Ulaya Alonso, amafanikiwa kunyakuwa makombe 2 ya michuano hiyo akiwa amecheza michezo 129 huku nahodha wa Munich yeye akiwa amenyanyua ndoo 1 na kucheza michezo 113 kwenye michuano hiyo ya Klabu Bingwa Barani Ulaya.

Comments

comments

You may also like ...