Header

Afande Sele atoa neno la busara kwa Belle 9 kufuatia msiba wa baba yake mzazi

Kufuatia msiba wa kumpoteza baba yake mzazi wa msanii wa bongo fleva ‘Belle 9’ mzee ‘Damian Nyamonga’ aliyefariki kwa ajali ya kugongwa na piki piki usiku wa juzi na mazishi kufanyika jana mida ya saa nane mchana ambapo wasanii baadhi walifika kumpa mkono wa pole msanii mwenzao.

Miongoni mwa wasanii waliofika ni pamoja na Stamina, Afande Sele, Jux, Edu Boy, G-Nako, Bright, timu ya Vitamini Music Group pamoja na baadhi ya ndugu jamaa na marafiki kitendo ambacho kulingana na matarajio ya Afande Sele amesema kuwa mategemeo kwake yalikuwa ni makubwa kulingana na idadi kubwa ya marafiki wanaojulikana kuwa na ukaribu na msanii mwenzao Belle 9 hasa kipindi cha furaha. Afande amesema kuwa kwa Belle 9 hiki ndicho kipindi cha kuwajua marafiki wenye nia njema, uhusiano wa kweli na wote wenye thamani kwake.

Msikilize Afande Sele alipokuwa akizungumza na Dizzim Online.

Comments

comments

You may also like ...