Header

Baada ya Kenya ‘Diplo’ kukinukisha Kampala, Uganda

Mshindi wa tuzo ya Grammy, rapa, muandishi wa nyimbo, na dj mmarekani maarufu mwenye makazi Los Angeles California, Diplo baada ya kufanya onyesho kubwa nchini Kenya na kujaza kwa kiasi kikubwa atua Kampala, Uganda.

Diplo ambaye ni pia ni dj wa msanii maarufu Major Lazer aliwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebbe jumatano mapema asubuhi(mida ya saa 10) akiwa na timu yake ya watu wasiopungua saba tayari kwa onyesho kubwa la siku ya tarehe 21 mwezi huu usiku wa ijumaa(Kesho) katika viwanja vya Golf Course Hotel.

Diplo na timu yake wakiwasili uwanja wa ndege

Diplo aliambatana na mjamaika-mmarekani Walshy Fire ambaye pia ni Dj, Mc, na mtayarishaji wa muziki mmoja kati ya watayakaotumbuiza katika onyesho hilo la msukumo wa Dancehall-raggae(Major Lazer) pamoja na madj wenzake Jillionare na Diplo ambao wote kwa pamoja wamekaribishwa katika jamhuri ya ndizi na timu ya Talent Africa wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Aly Allibhai, ambaye pia mratibu wa tukio hilo.

Aly Allibhai akiwa na Diplo pamoja na Walshy Fire uwanja wa ndege wa Entebbe

Diplo amefanikisha kazi nyingi kubwa za wasanii wa kubwa duniani ambao ni pamoja na Justin Beiber, Beyonce, Madonna, Chris Brown, Usher, Snoop Dogg na wengine wengi.

Hata hivyo Diplo aliitumia siku yake ya jana yote ya akiutazama na kuutembelea mji wa Jinja na Allibhai ndiye alisimamia nakuongoza ziara yake hiyo.

Comments

comments

You may also like ...