Header

Dame Dash atangaza kusukwa kwa filamu ya historia ya Roc-A-Fella Records

Mambo mengi ambayo hayajawahi kusema kuhusu Roc-A-Fella Records enzi ikiwa kwenye chati, yataonekana kwenye filamu (biopic) ijayo, kwa mujibu wa muasisi mwenza wa label hiyo, Damon Dash.

Dash amedai kuwa bado anaendelea kuitengezea filamu hiyo na itaelezwa katika mtazamo wake mwenyewe. “There’s a lot that people didn’t see and that would be the part I’d be showing,” amesema Dash kwenye interview. “So you don’t know what I’m going to show you. Why would I just make a re-creation of what everyone saw? I want to make things that no one knew.”

Label hiyo ilianzishwa mwaka 1996 na Jay Z, Kareem “Biggs” Burke na yenye mwenyewe Dame Dash na ndiyo iliyowatoa wasanii Hov, Kanye West, Cam’ron, Memphis Bleek, Beanie Sigel, DJ Clue na wengine.

Dash alijiondoa kwenye label hiyo bila kutangaza akidai kuwa hakujisikia kuendelea nayo tena.

Comments

comments

You may also like ...