Header

Diamond Platnumz atangaza siku ya Chibu Perfume

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Kutoka Tanzania na staa wa ngoma ‘Marry you’ aliyomshirikisha staa wa RnB kutoka Marekani ‘Ne-Yo’ amezidi kupanua wigo wake zaidi kama msanii na mfanyabiashara. Baada taarifa kutoka kwa meneja wake ‘Sallam Sk’ kuhusu ujio wa kikubwa kwenda kwa mashabiki kati ya Diamond Platnumz na rapa mmarekani ‘Future’ hatimaye siku rasmi ya kuigia sokoni kwa manaukato ya Diamond(Chibu Perfume) imetangazwa rasmi.

Kupitia ukurasa rasmi wa Instagram wa msanii Diamond, amethibitisha kuwa tarehe 21, Mwezi huu siku ya Ijumaa(kesho) ni siku rasmi ya kuigia sokoni kwa manukato yake(Chibu Perfume) na kuwataka watu wote wanaojali kupendeza na kunukia wasisite kujichukulia kwa matumizi ya kuongeza thamani ya muonekano wa mtu na utanashati wake.

Chibu Perfume by Diamond Platnumz

ATTENTION LADIES AND GENTLEMAN!!!! JUS WANTED TO LET YOU KNOW THAT @CHIBUPERFUME WILL BE OFFICIALLY OUT THIS FRIDAY!!! #TheScentYouDeserve” Alipost Diamond Platnumz.

Hata hivyo katika mazungumzo na Dizzim Online wiki iliyopita Sallam na Diamond wakiwa location nchini Afrika Kusini katika kushoot tangazo la manukato hayo alithibitisha kukamilika kwa tangazo hilo maalum la manukato hayo hivyo kinachotegemewa ni taarifa kuwafikia wapenzi wa manukato kuwa ni wapi kila mmoja wenye mahitaji wafike kufurahia bidhaa hiyo inayotazamiwa kuwa na ubora.

Comments

comments

You may also like ...