Header

Mastaa wawili kutoka Kenya wagusa anga ya followers millioni moja

Katika maisha ya umaarufu mitandao ya kijamii hasa kipindi cha utandawazi kuzidi kukua kwa kasi imezidi kuwa na nguvu kiasi cha wahusika wenye majina makubwa kuweza kufanya biashara kupitia akauntu zao wanazo tumia katika kuwa karibu zaidi na mashabiki mitandaoni.

Afrika Mashariki kwa kujumuisha Tanzania, Kenya na Uganda zimetajwa kuwa ni miongoni mwa nchi zenye matumizi makubwa ya huduma ya intaneti. Na sasa kwa mujibu wa akaunti za Instagram  za mastaa imeonekana kuwa mchekeshaji ‘Eric Omondi‘ na mwanamitindo, muigizaji na mfanyabiashara ‘Huddah Monroe’ wamekuwa watu maarufu wa kwanza nchini Kenya kufikisha wafuasi milioni moja.

Akaunti rasmi ya Instagram ya Mchekeshaji Eric Omondi

Akaunti ya Instagram ya Huddah Monroe

Hata hivyo watu maarufu wengine nchini Kenya walioko njiani kufikia idadi kubwa ya wafuasi milioni moja ni kundi la waimbaji la Sauti Sol ambao wana wafuasi 911k.

 

 

Comments

comments

You may also like ...