Header

Steve Nyerere awasaliti Bongo Movie

Jana wasanii wa Filamu hapa Bongo waliandamana kati kati ya jiji la Dar es salaam wakishinikiza Serikali kuchukua hatua ya kutokomeza filamu za kigeni ambazo zinaingia nchini Kinyemela ombi ambalo waliliwasilisha mapema mwezi huu kwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda,Lakini jambo hilo limepingwa vikali na mchekeshaji Steve Nyerere.

Steve Nyerere amesema tangia zamani filamu za kigeni zilikuwa zinatazamwa sana wakati huo hata Bongo Movie walikuwa bado hawajaanza kuigiza lakin i walivyoingia kwenye tasnia rasmi watu wakaanza kupenda movie zetu hadi leo wasanii wana majina makubwa sasa maandamano ya nini?alihoji Steve Nyerere.

Kwanza sijakubaliana na maandamano yaliyofanyika,kwanza niwe muazi tuu mambo mengine yanafanywa nje ya sheria,mimi siwezi kukubaliana heti kuna maandamano na mimi niende hilo haliwezekani ndiyo maana hujaniona kwenye maandamano“Amesema Steve Nyerere na kuendelea kusisitiza kuwa soko la filamu halijafa nchini

Kwanza tunapozungumza filamu za nje ndiyo zinaua soko la bongo Movie ni uongo,sisi zamani tulikuwa tumnaangalia movie za akina Arnold na Jack Chain na baada ya kuanza Movie zetu tukaanza kuchukua majority na ndiyo hapo tukaanza kukua,sasa kusema heti soko linakufa kwa ajili ya movie za kigeni ni uzushi,Tumepambana na movie za kinaijeria tukashinda,zikaja za kijapani na kichina tukashinda,wakaja waghana tukashinda wakaja akina Lulu wakashinda hadi tuzo.Niseme tuu Movie ni biashara je utaniuzia Movie yako mbovu kwa Elfu sita wakati movie nzuri inauzwa kwa bei rahisi kwa wamachinga,Mtanzania hawezi kununua filamu ya elfu 6 na pili tuongeze ubora hapo uzalendo utauona“Alisema Steve Nyerere kwenye mahojiano yake na Global TV.

Awali maandamano ya wasanii wa Filamu yalitangazwa kwa wasanii wote wanaohusika kwenye Kiwanda cha Bongo MOVIE waandamane kudai haki yao jambo ambalo halikuungwa mkono na Wasanii wote akiwemo Steve Nyerere.

 

 

Comments

comments

You may also like ...