Header

Timu za LaLiga zaendeleza ubabe kwenye michuano ya Klabu bingwa ulaya

Michuano ya Klabu Bingwa barani ulaya maarufu kama (UEFA Champions League) inakaribia ukingoni ambapo mpaka sasa bado timu za Uhipania zinaendelea kunyanyasa vilabu vingine kwenye michuano hiyo ambayo mpaka kufikia hatua hii ya Nusu fainali tayari timu mbili zimeingia huku mbili nyingine zikitoka Italia na Ufaransa.
Klabu hizo zilizofuzu kutoka Hispania ni Real Madrid ambao waliwavurumisha Bayern Munich na Atletico Madrid ambao waliwatupa nje mabingwa watetezi wa EPL Leicester city,Na klabu nyingine zilizofuzu ni Klabu ya Monaco kutoka Ufaranza ambao wamewagonga Borussia Dortmund nje ndani na Vibibi vya Torino Juventus nao wamefuzu kwa kuwagaragaza Mabingwa mara tano wa michuano hiyo FC Barcelona.
Mechi zitakuwa kali na ni vigumu sana kutabiri nani ataingia fainali, lakini Hispania kwa namna yoyote ile lazima itapeleka timu moja au zote mbili kwa pamoja kama ilivyowahi kutokea 2013-2014 na 2015-106 Madrid anakutana na Atletico na Atletico anakufa mechi zote mbili.
Draw ya kupanga mechi hizo za hatua ya Nusu fainali zitafanyika Ijumaa hii kesho huko mjini Nyon, Switzerland.

Comments

comments

You may also like ...