Header

Afya ya Method Mwanjali wa Simba bado ni utata

Beki tegemeo wa Simba, Method Mwanjali leo amefikisha siku 69 tokea aumie na huenda akakaa nje ya uwanja msimu huu wote baada ya kuumia kwenye mchezo dhidi ya Prisons ya Mbeya.
Mwanjali raia wa Zimbabwe, aliumia Februari 11, mwaka huu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Prisons ya Mbeya kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam,Hadi sasa hajaanza mazoezi mepesi na Simba imebakiza mechi tatu tu za Ligi Kuu Bara kumaliza msimu.
Mwanzoni mwa mwezi uliopita klabu ya Simba iliahidi kuwa mchezaji huyo atakuwa fiti ifikapo mwezi Aprili lakini mpaka sasa bado hakuna taarifa yoyote rasmi kutoka kwenye klabu hiyo na Mwanjali haonekani akifanya mazoezi na kikosi hicho.
Hii inaashiria hatakuwa fiti hata kama ataanza mazoezi wiki moja ijayo kutokana na hali ilivyo na kama akirudi, huenda mechi ya mwisho kabisa Mwanjale amekuwa tegemeo katika kikosi cha Simba katika suala la ulinzi hadi alipoumia.

Comments

comments

You may also like ...