Header

Janvier Bukungu amlilia Method Mwanjali.

Beki wa kati wa Wekundu wa Msimba Method Mwanjali, akiendelea kuuguza maumivu ya kifundo cha mguu, beki wa kulia wa kikosi hicho, Janvier Bukungu, amesema akimkosa swahiba wake huyo anashindwa kutimiza kwa ufasaha majukumu yake.

Akizungumza na Gazeti la Michezo la Bingwa  Bukungu alisema pamoja na kuwa ana imani na mabeki wengine, Murshid Jjuuko na Novarty Lufunga, lakini  wakicheza na Mwanjali inanoga kutokana na kujenga uhusiano mzuri wa kukaba nakutimiza majukumu yetu kiwanjani.

“Simba ina mabeki wazuri sana, kila mmoja ni muhimu katika timu, lakini uwepo wa Mwanjali tunafanya vizuri,” alisema Bukungu

Beki huyo aliumia kwenye mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Tanzania Prisons iliyofanyika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam na Simba kushinda mabao 3-0.

Comments

comments

You may also like ...