Header

Joseph Omog” sina wasi wasi na point tatu za Kagera hata zikichukuliwa ubingwa wetu”

Kocha wa Simba Joseph Omog amesema hata kama watapokwa pointi tatu za Kagera bado timu yake inaweza kuwa mabingwa msimu huu endapo watashinda mechi zao tatu zilizobaki.

Akiongea na Goal.com Omog raia wa Cameroon ameiambia kinachompa matumaini ni kutokana na udhaifu waliokuwa nao wapinzani wao Yanga ambao licha ya kuwa na michezo miwili ya viporo lakini timu yao ina matatizo mengi inayowafanya wasiwe na uwezo wa kushinda mechi zote zilizo baki.

Hii ni ligi na ushindani umekuwa mkubwa sidhani kama Mbeya City au Mbao watakubali kufungwa na Yanga ukizingatia na zenyewe zinahitaji matokeo ili kujiweka kwenye nafasi nzuri hivyo bado ninaamini Simba inayo nafasi ya ubingwa msimu huu hata kama tutapokonywa pointi tatu za Kagera,” amesema Omog.

Kocha huyo aliyeibadilisha Simba kwa kiasi kikubwa msimu huu na kuileta kwenye ushindani iliyokuwa nao zamani amesema mikakati yake ni kuhakikisha anawaandaa vizuri wachezaji wake ili waweze kucheza vizuri na kushinda mechi zao.

Comments

comments

You may also like ...