Header

Madee azipa kisogo Kolabo

Hivi unafahamu kwamba Msanii kutoka Tip top connection Madee ni moja kati ya wasanii wasiopenda kushirikishwa kwenye wimbo wowote na msanii yoyote? kama hujui kuhusu hilo ukweli wote  ni huu hapa.

Madee amefunguka kwamba mimi sitaki kushirikishwa na msanii yoyote iwe Tanzania au nje ya Tanzania , amesema kwa upande wake anaona hakuna umuhimu wa kushirikishwa ndo nilivyoamua na kama kuna mtu ana ndoto za kumshirikisha Madee kwenye wimbo wowote aondoe mawazo ayo

Ameongeza kuwa ata mimi kumshirikisha mtu sifanyi hivyo kwanza naona kila wimbo naona naenea mwenyewe na kama ukiona mimi nimemshirikisha mtu basi ujue kuna swala kubwa sana ndo nitamshirikisha msanii , kwanza ata album yangu naweza kuachia ngoma zote
nipo mwenyewe ila kwa sasa mpango ni kuachia compilation album mimi na dogo janja ambapo tarehe bado kutangaza,”Alisema Madee.

Mkali huyo kutoka Tip top connection kwa sasa anafanya vizuri sana na wimbo wake hela unaobamba na kushika chati kwenye radio na tv nyumbani na nje ya Tanzania

Comments

comments

You may also like ...