Header

Hivi ndivyo vitu vinavyosababisha Ben Pol ashindwe kumiliki wasanii wake.

Muziki wa Tanzania umekua kwa nafasi kubwa na tumeshuhudia wasanii kadhaa wakubwa wakiwa na label zao ambazo nazo zinawasimamia wasanii wachanga au wasanii ambao wameshindwa kujiendeleza wao wenyewe hivyo wameungana kuusimamisha vizuri muziki wa Bongo Fleva.

Ben Pol ni miongoni mwa wasanii wakubwa wa Rnb na wenye majina makubwa zaidi Tanzania kutokana na muziki wake kusifika kwa uzuri na kusikilizika na kila rika bila kujali itikadi ya umri wala jinsia zaidi na ukubwa wa muziki wake umefanya muziki wake kuvuka hadi mipaka ya Tanzania.

Ben Pol ametoa sababu ambazo kwake anaamini atachelewa kumiliki label au wasanii watakaokua chini yake>>’Bado nataka kushamili zaidi,ukianza kummanage halafu wote mnakwama inakua sio sawa,inatakiwa kuwa power yako iwe imara zaidi’

‘Bado sijawa na Capital ambayo inaenda nje ya mimi ya kusema niivest kwa msanii,sijakua na ziada ya kufanya hivyo kusema kweli,naweza kufanya biashara zingine naikosa ile ziada maana inabidi hela ibakie ili uweze kufanya hivyo’ – Ben Pol.

Source XXL ya Clouds FM.

Comments

comments

You may also like ...