Header

Barack Obama arudi mbele ya jamii kwa style hii

Ni miezi mitatu tangu amkaribishe Rais wa Marekani Donald Trump na yeye kwenda mapumziko aliyekuwa Rais wa Marekani ‘Barack Obama’  huu ndio upande ambao wengi wanaomfatilia wanahitaji kumuona sana tofauti na ilivyokuwa kipindi chake cha uongozi.

Obama ameamua kurudi kwenye maisha ya kuonekana zaidi kwenye jamii ambapo ujio wake utampeleka mjini Chicago kwa lengo la kuzungumza na wanafunzi katika chuo kikuu cha Chicago(Univesity of Chicago) kuhusiana na umoja na ushirikiano mwema wenye faida katika jamii kama moja ya tukio lake la kwanza lenye faida kwa jamii tangu atoke Ikulu ya Marekani mwezi Januari mwaka huu.

Hata hivyo kwa mijibu wa ujumbe uliotumwa siku ya Ijumaa Rais mstaafu ataonekana kwenye jukwaa la utoaji elimu ya kijamii akiwa na idadi ya wanafunzi 6 wa shule ya sekondari, chuo na wahitimu wa vyuo kama wasemaji wake wakuu na tukio hilo litarushwa katika vituo vya televisheni.

Comments

comments

You may also like ...