Header

Bodi ya filamu yakanusha uvumi

Bodi ya filamu nchini Tanzania imekanusha taarifa zinaeondelea kusambazwa katika mitandao ya kijamii na baadhi ya watu wenye nia ya kupotosha kwa mashali yao binafsi.

Kupitia barua rasmi kutoka kwenye bodi ya filamu imeeleza kuwa, taarifa za serikali kuzuia kwa maksudi uingizaji, usambazaji na uuzwaji wa filamu za kigeni nchini kwa lengo la kulazimisha watanzania kungalia filamu za ndani uvumi ambao umeshamiri zaidi tangu kuandamana kwa waigizaji wa filamu Tanzania(Bongo Movie) wakishinikiza kufungwa kwa biashara ya filamu za kigeni.

Barua kutoka Bodi ya filamu

Hata hivyo vugu vugu hilo limeweka sura ya tofauti kwa wadau na mashabiki hata baadhi wakishauri kuwa tasnia ya filamu bado inao uwezo wa kuboresha kazi zao kiasi cha wahitaji kuongezeka na wahusika kupata masilahi ya kujitangaza kimataifa kwa kazi zenye ubora.

Comments

comments

You may also like ...