Header

Chelsea yatinga fainali ya FA kibabe

Vinara wa  Ligi kuu nchini Uingereza Chelsea wametinga fainali ya michuano ya FA baada ya kuwachapa majirani zao Tottenham Hotspur kwa  magoli 4-2 kwenye dimba la Wembley.

Chelsea walipata goli la kwanza kupitia kwa mbrazili Willian ambaye alifunga kwa mpira wa adhabu ndogo kwenye dakika ya 7 kipindi cha kwanza badae mshambuliaji wa Spurs, Harry Kane alisawazishia Tot kwenye dakika ya 17 kabla ya kipindi cha kwanza kuisha Willian alipatia Chelsea goli la 2 mnamo dakika ya 43.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na timu zote kushambuliana kwenye dakika ya 52 Dele Alli alisawazishia Tot na kufanya matokeo kusomeka 2-2 ndipo Kocha wa Chelsea Antonio Conte alifanya mabadiliko ya kumwingiza Diego Costa na Eden Hazard na kufika dakika ya 74 Hazard alifunga goli la 3 na Nemaja Matic akafunga goli la 4 mnamo dakika ya 80

Kwa matokeo haya yanaifanya Chelsea kutinga fainali ya FA huku wakimsubili mshindi kati ya  Arsenal na Manchester City hapo kesho.

Comments

comments

You may also like ...