Header

David Luiz aihofia Tottenham Hotspur

Beki wa Chelsea Mbrazili  David Luiz ameitaja Tottenham Hotspur kama timu ya watu wakutisha kuelekea mechi yao ya Kombe la FA nusu fainali katika uwanja wa Wembley.

Spurs wamejiimarisha kuwa moja ya timu yenye upinzani mkubwa kwa Chelsea kwenye Ligi Kuu nchini Uimgereza katika mbio za kuwania Ubingwa msimu huu, wakipunguza pointi kutoka 10 hadi kubaki 4 tangu kuanza kwa Aprili

Akizingumza na Gazeti la  London Evening Standard amesema kuwa “Kwangu mimi ni timu nzuri sana, yenye kocha mahiri Mauricio Pochettino. Ni timu ya watu wenye nguvu katika ligi. Wachezaji wote 11 ni majitu ya kutisha. Nawapenda kwa kweli,”

Luiz ameanza mechi 28 Ligi Kuu Uingereza kwa Chelsea msimu huu, kwa kiwango chake amepata ameingia kwenye timu  ya PFA ya mwaka

Comments

comments

You may also like ...