Header

Diamond Platnumz atoa wito kwa wasanii wa jinsi ya kutumia umaarufu wao

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania Naseeb Abdul a.k.a Diamond Platnumz ashauri kikubwa kwa wasanii mapema jana alipokuwa katika uzinduzi wa manukato yake(Chibu Perfume) uzinduzi uliofanyika GSM Mall barabara ya Pugu jijini Dar es salaam.

Akizungumza na wadau na waandishi wa habari, Diamond amesema kuwa wasanii wanao wajibu mkubwa wa kutumia umaarufu wao katika vitu vyenye tija hivyo wasisite kujijenge katika mitazamo ya namna ya kuwa mchango kwa faida yao na jamii zao.

“nafikiri tutumie umaarufu wetu katika sehemu chanya yaani chanya kwa maana kwamba isiwe basi umaarufu au influence tuliyoipata tukaitumia katika mambo ambayo hayana maana na hayaleti tija katika jamii…mimi ni mtu ambaye sometimes sipendagi kusubiri eti mpaka wanasiasa wafanye lakini hata mimi kama msanii kama kitu naweza kukifanya basi niko radhi nikifanya ili kuonyesha kwamba unaweza kuwa msanii lakini ukafanya kitu ambacho kinaleta tija kwenye jamii” Alisema Diamond Platnumz.

Hata hivyo Diamond amesema hivyo kufuatia mambo kadhaa ambayo amekuwa akiyafanya ikiwa ni pamoja na kujenga msikiti, kama moja ya njia ya kuirudishia shukrani jamii iliyomfikisha nafasi aliyopo.

 

Kusikiliza aliyoyasema yote Diamond Platnumz katika uzinduzi wa manukato yake(Chibu Perfume) itazame video hapa chini.

 

 

Comments

comments

You may also like ...