Header

Foby ampeleka Hanscana Zanzibar

Picha kwa hisani ya Instagram

Msanii 'Foby'

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania ‘Foby’ aliyefanya vizuri na wimbo wake ‘Star’ wimbo uliowafanya wengi kutamani kumsikia zaidi na zaidi aachia kazi nyingine amabayo ina kila dalili za kufanya vizuri kutokana na ubora wake.

Kutoka katika upishi wa C9 kanjenje katika studio za C9 Records kwa mara nyingine tena Foby amekuja na ujio wa ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina ‘Ila’ wimbo unaonekana kuwa na wazo la mapenzi ndani yake kwa namna nyingine ya tofauti na ile ya wimbo wa ‘Star’.

Katika kukamilisha wimbo huo C9 Kanjenje kama mtayarishaji wa audio na director Hascana wamehusika kwa asilimia kubwa ya ujuzi na mwisho kazi ikamilika ambapo video ya wimbo huu imeshootiwa Zanzibar.

Comments

comments

You may also like ...