Header

Lil Wayne: Jay Z ni rafiki anayenisaidia kwenye vita yangu na Cash Money

Lil Wayne ameamua kutolea ufafanuzi tetesi za kuwa amejiunga na label ya Jay Z, Roc Nation. Kwenye mahojiano na Skip Bayless, rapper huyo amedai kuwa Jay Z amekuwa rafiki yake wa karibu anayetaka kumsaidia katika vita yake na Cash Money mahakamani.

“Jay ni mtu mzuri tu,” amesema Wayne. “Hakukuwa na kitu chochote zaidi ya kitu kidogo tu. Rafiki kwa rafiki, nataka tu kukusaidia. Hivyo tu. Hivyo ndio ilikuwa. Nataka tu nikusaidie kwa lolote ninaloweza kufanya. Kwa sasa ataenda kunisaidia kwa vyovyote atakavyoweza.”

Hata hivyo hiyo haimaaishi kuwa vita yake na Cash Money imekwisha. “Hapana. Hatujamaliza bado,” alisema. “Tunaendelea kulishughulikia hilo. Lakini Jay ni mtu mzuri na anataka tu kunisaidia. Atakuwa akinisaidia.”

Comments

comments

You may also like ...