Header

Breaking:Msanii Mucky wa Makomando afiwa na mama yake mzazi..

Taarifa ambayo imetufikia usiku wa April 22 ni hii ya mmoja kati ya wasanii wanaounda kundi la Makomando aitwae Mucky kuondokewa na mama yake mzazi,taarifa kamili juu ya chanzo cha kifo cha mama yake haijafahamika bado,DizzimOnline inatoa pole kwa ndugu,jamaa na marafiki walioguswa na msiba huu pia tunamuomba Mungu amjaalie Mucky wepesi kwenye kipindi hiki kigumu kwake.

Mucky akiwa na Mama yake enzi ya uhai wake.

Mucky na Fred Wayne ni wasanii wanaoounda kundi la Makomando ambalo wamefanikiwa kutoa nyimbo kadhaa zilizofanya vizuri zaidi,hii ni moja kati ya singo zao walizotoa hivi karibuni,kwenye post ya Fredwyne kwenye instagram ameandika maneno ya kumpa faraja Mucky na ameandika >>’Mapenzi uliyokua nayo juu yake haya elezeki hata mara moja mimi najua kwa kuwa ni mtu wa karibu mnoo kwako pole sana @muckycomando jikaze ndugu yangu najua hiki ni kipandi kigumu kwako na kwetu pia nikiwa kama mwanafamilia PUMZIKA kwa amani mama yetu (R.I.P.MAMA MUCKY) ratiba zingine tutawataarifu ndugu zetu‘ – Fred Wayne.

 

Comments

comments

You may also like ...