Header

Uongozi wa timu ya Simba umefikia hatua hii nyingine kubwa leo April 22…

Kwenye mgogoro au vitu vingi vinavyozungumzwa kwenye upande wa michezo sasa hivi ni pamoja na hii ya team ya Simba Sports Club juu ya kupambana na zile point ambazo walikua wamepatiwa dhidi ya mgogoro uliopo kati yao na Kagera Sugar.

April 21 Simba waliandika barua ya kuomba maandamano ya amani kuelekea kwa Waziri wa habari,Utamaduni,Michezo na Sanaa,maandamano yalipangwa kufanyika Jumanne ijayo ya April 25.

 

Taarifa nzuri ni kuwa timu ya Simba leo wamekutana na Waziri Mwakyembe ambaye ndiye Waziri mwenye dhamana ya Michezo na kuzungumza nae,kupitia ukurasa wa twitter wa Simba wameandika >>’Uongozi wa Simba wakutana na Waziri Mwenye Dhamana ya Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe’

Comments

comments

You may also like ...