Header

Alichoandika Jerry Muro baada ya TFF kumfungia Haji Manara

Baada ya tamko la Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF) kutangaza kumfungia Ofisa habari na mawasiliano wa Klabu ya Simba Haji Manara,hatimae msemaji wa zamani wa Klabu ya Yanga Jerry Muro amempokea kwa mbwembwe zote uraiani.

Jerry Muro ambae nae alipatwa na kifungo kama hicho cha kutokujihusisha na mpira wa miguu ndani na nje ya Tanzania amemkaribisha Haji Manara mapema baada ya kupewa adhabu na TFF kwa kuwambia watanzania wawaache wawili hao wapumzike kwani wamelitumikia soka vya kutosha.

Mtuache sasa tupumzike, tuliyofanya kwa taifa hilo haswa kwenye mpira nadhani yametosha, Waswahiba karibu kijiweni @hajismanara“Ameandika Jerry Muro kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Haji Manara amepewa adhabu ya kutokujihusisha na Soka nje na ndani ya Tanzania  kwa muda wa mwaka mmoja na faini ya Milioni 9.

Comments

comments

You may also like ...