Header

Bifu linaendelea; Vin Diesel amvimbia The Rock

Baada ya bifu kali iliyodumu kwa muda mrefu Mwigizaji Vin Diesel amefunguka kwa mara ya kwanza na kusema katika maisha ya kawaida anaweza kupigana na kumshinda mwigizaji mwenzake Dwayne johnson (The Rock).

Licha ya Tarifa za awali zilizotolewa na rafiki yao Tyrese wiki moja iliyopita kuwa wawili hao hawana Bifu kama watu wanavyodhani ukweli ni kwamba Vin Diesel bado anamtafuta The Rock kwenye maisha ya Kawaida kwani anaamini kuwa mbabe huyo hawezi kumfanya chochote kile na yupo tayari hata kupangiwa pambano la wazi kuzichapa.

Kupitia mtandao wa Vanity Fair habari zinaeleza kuwa Vin Diesel anajitahidi kupotezea bifu hilo ila anaumizwa na marafiki wao wa karibu ambao wanatoa taarifa za kupotosha umma kuwa amefyata mkia kwa mbabe huyo ambae hatishiki kwa lolote.

Mwanzoni mwa mwezi August mwaka jana Studio ya Universal ilitangaza kuwa Dwayne Johson (The Rock) na Vin Diesel wamemaliza bifu lao ambalo liliibuka wakati wakirekodi movie ya nane ya mwendelezo wa movie za Fast and Furious,ila sasa tupo miezi tisa mbele na inaonekana bado bifu linaendelea na wala dalili ya kupoa haipo.

Source:http://www.vanityfair.com

Comments

comments

You may also like ...