Header

Drake amjibu mrembo aliyetangaza ana ujauzito wake mitandaoni

Wiki hii habari kubwa ya burudani kutoka majuu ni ile ya Mwanamitindo aliyejulikana kwa jina la Layla Lace kuvujisha Chats zake na Drake na kulalamika kuwa ametelekezwa na Mkali huyo baada ya kumpa ujauzito kwani hapokei Simu wala hajibu meseji zake,hatimae Drake amefunguka ukweli wote baada ya kuzipata habari hizo.

Image result for Layla Lace

        Mrembo Layla Lace aliyedai kupewa mimba na Drake

Drake amesema taarifa hizo amezipata na hata huyo aliyesambaza uzushi huo hamjui ni uongo tuu anaojaribu kuutengeneza ili aweze kupata Kiki kwenye mitandao ya kijamii lakini vitu vyote alivyoongea vinafaa kupuuzwa.

Hata hivyo Uongozi wa Drake umesema upo mbioni kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mrembo huyo kwa kosa la kumchafua Drake.

Comments

comments

You may also like ...