Header

Manchester United yaendeleza ubabe Uingereza

Manchester United yaendeleza wimbi la ushindi baada ya wikiendi iliyopita kuichapa Chelsea na leo imechukua tena pointi tatu nyumbani kwa Burnley kwa kuiadhibu goli 2-0.

Wafungaji wa Mashetani wekundu leo walikuwa Antonio Martial ambaye alitupia dakika ya 21 na Captain Wayne Rooney mnamo dakika ya 39 alipatia timu yake goli la pili na kuitimisha ushinndi wa Man U.

Kwa ushindi wa leo United wameendelea kushikiria nafasi ya 5 wakiwa na alama 63 mbele ya jirani zao Man City wakiwa na Alama 64 huku wakiwa na nafasi ya 4.

Comments

comments

You may also like ...