Header

Sanchez aipeleka Arsenal Fainali

Arsenal imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya michuano ya FA baada ya kuitupa nje Manchester City kwa kuiadhibu goli 2-1 kwenye dimba la Wembley jijini London.

Mchezo wa nusu fainali ulikuwa mgumu na wenye kuvutia sana kwani mpaka kipindi cha kwanza kinaisha milango yote ilukuwa miguu kwa timu zote mbili, kipindi cha pili kilianza kwa kasi sana na kwenye dakika ya 62 Aguero alipatia City bao la kuongoza Arsenal walishambulia kwa kasi na kuweza kusawazishakupitia kwa beki wa kushoto,Monreal kwenye dakika ya 71.

Mpaka dakika 90 zinaisha mpira ulikuwa 1-1 ndipo zikaongezwa dakika 30 za ziada na kwenye dakika ya 100 Sanchez alifunga goli la 2 kwa Arsenal na la ushindi na kuifanya kutinga Fainali.

Ushindi wa leo alioupata Arsenal unamfanya kutinga fainali ambayo atacheza na Chelsea kwenye dimba la Wembley tarehe 27 may mwaka huu.

Comments

comments

You may also like ...