Header

Simba chali; Kagera Sugar yarudishiwa pointi 3 na TFF

Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF) limetangaza kuipora Simba pointi tatu na mabao matatu ambayo ilipewa kutokana na mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar baada ya kamati yao .

Wiki mbili zilizopita Simba ilipoteza mchezo dhidi ya Kagera Sugar kwa kufungwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara lakini baadaye ilikata rufaa ikipinga Kagera kumtumia mchezaji Mohamed Fakhi ikidai alikuwa na kadi tatu za njano, ndipo ikapewa ushindi huo kupitia Kamati ya Saa 71.

Mara baada ya kamati hiyo kuipa Simba pointi Kagera ikaomba kupitiwa upya kwa suala hilo na ndipo TFF ikatangaza kuwa suala hilo sasa litakuwa chini ya Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF ambayo ndiyo imetoa maamuzi hayo.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari juu ya uamuzi huo, Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa amesema kuwa kuna sababu kadhaa zimechangia kuchukuliwa kwa maamuzi hayo ambapo alianza kwa kusema…

Malalamiko ya Simba hayakuwasilishwa kwa wakati muafaka tangu mchezo ulipochezwa, malalamiko yao hayakuwa katika njia ya maandishi, rufaa ya Simba haikulipiwa ada, kikao cha Kamati ya Saa 72 kilikosa uhalali kutokana na kuwashirikisha watu ambao hawana uhalali wa kuwa kwenye kikao,Kutokana na sababu hizo kamati imeamua kufuta maamuzi yaliyochukuliwa na Kamati ya Saa 72 na kurejesha matokeo kama yalivyokuwa, pia kamati imemuagiza katibu mkuu wa TFF kuwapeleka baadhi ya wajumbe wa bodi ya ligi katika Kamati ya Maadili ya TFF kwa kosa la kwenda kinyume na kazi zao,” Alisema Katibu mkuu wa (TFF) Selestine Mwesigwa.

Comments

comments

You may also like ...