Header

Simba uso kwa uso na Azam FC; Soma ratiba kamili ya kombe la ASFC

Leo shirikisho la Soka nchini Tanzania TFF limepanga ratiba ya michezo ya nusu fainali ya kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) ambapo kwenye droo wababe wawili wa jiji la Dar es salaam klabu ya Simba na Azam FC zitakutana.

Azam FC watakutana na wakali hao wa Msimbazi tarehe 29 ya mwezi huu Aprili kunako uwanja wa Taifa Dar es salaam huku mchezo mwingine utakuwa ni kati ya Mabingwa watetezi wa Ligi kuu Tanzania Bara Yanga dhidi ya Mbao FC ya jijini Mwanza,Mchezo utakaopigwa Aprili 30 ya mwezi huu ndani ya CCM Kirumba.

Comments

comments

You may also like ...