Header

Simbu ahaidi kupeperusha vyema Bendera ya Tanzania

Mwanariadha pekee wa Tanzania Alphonce Felix Simbu, leo Jumapili ataibeba bendera ya Tanzania kwenyemashindano ya London Marathon yanayofanyika jijini London.

Akiongea na kituo cha East Africa Radio amsesema kuwa amaejipanga kuakikisha anashinda hiyo medali kwani nimejiandaa vya kutosha naomba dua na sala za Watanzania.

“Nitapambana kwa nguvu zangu zote…nina imani nitashinda kwani nimefanya mazoezi ya kutosha na nina ari na moyo wa kushinda. Naomba sala za watanzania wote ili niweze kuleta medali nyumbani” amesema Simbu

Alphonce, ambaye ni Mtanzania wa kwanza kushinda medali ya dhahabu katika mashindano maarufu ya Standard Chartered Mumbai Marathon, anatarajiwa kuwapa wakati mgumu manguli wa riadha ulimwenguni wanaoshiriki mbio hizo za London akiwemo Muethiopia Kenenisa Bekela pamoja na wengine kutoka Ethiopia na Kenya

Comments

comments

You may also like ...