Header

Tanzania,Ethiopia hoi mbele ya Wakenya kwenye mbio za London Marathon

Mtanzania Alphonce Felix Simbu ameshika nafasi ya tano kwa kusua kusua kwenye mbio za London Marathon zilizofanyika mchana wa leo jijini London, Uingereza akiwa nyuma ya wakenya watatu na muethiopia mmoja.

Daniel Wanjiru kutoka Kenya aliibuka kinara wa mbio hizo akitumia muda wa saa 02:05:48, nafasi ya pili ikichukuliwa na Kenenisa Bekele wa Ethiopia aliyetumia muda wa saa 02:05:57.

Nafasi ya tatu ya mbio hizo imeenda kwa mkenya mwingine Bedan Karoki aliyetumia muda wa saa 02:07:41, nafasi ya nne ikaenda kwa mkenya Abel Kirui akitumia muda wa saa 02:07:45, na namba tano ikienda kwa mtanzania Alphonce Simbu aliyetumia muda wa saa 02:09:10.

Comments

comments

You may also like ...