Header

Vita ya Ronaldo na Messi yapamba Moto usiku huu

Usiku huu majira ya saa 3:45 usiku kwa saa za kibongo, ndani ya dimba la Santiago Bernabeu, litapigwa bonge la mechi la kibabe, kati ya miamba miwili ya soka nchini Hispania na duniani kwa ujumla, Real Madrid na Barcelona.

EL Clasico. Ndiyo, huo ni mtihani mgumu zaidi kwa Real Madrid msimu huu. Na kitakachosababisha ugumu wenyewe ni kwamba, Barcelona kwa hali yoyote ile itazihitaji pointi tatu pale Bernabeu.

Barcelona tayari imeshaondolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, kitakachowaokoa na aibu ya msimu ni kubeba taji la La Liga, lakini swali lililopo ni jinsi gani Wakatalunya hao watakavyoweza kuizamisha Madrid yenye fomu nzuri msimu huu.

El Clasico pamoja na michezo mingine iliyosalia, ni nafasi ya mwisho kwa Barca. Na iwapo wamejiandaa vyema, tuitarajie Barcelona tofauti usiku wa leo.

Comments

comments

You may also like ...