Header

Keisha afunguka makubwa juu ya ukimya wake kwenye muziki

Msanii wa muziki kutoka Tanzania Keisha ni moja kati ya wasanii wa kike ambao wanauwezo mkubwa sana kwenye uimbaji lakini cha kushangaza bado haonekani kwa kipindi kirefu kwenye muziki bila kujua ni kipi kimemsibu hali ambayo imemfanya apoteze baadhi ya mashabiki wake na hatimae amefunguka chanzo cha ukimya wake.

Keisha akiongea na Dizzim Online amesema ukimya wake kwenye muziki unapelekewa na mambo makubwa mawili ambayo ni malezi ya mtoto wake ambae bado mdogo na kingine ni ubize na masomo.

Ukimya wangu umesababishwa na mambo makubwa mawili moja la malezi ujue nina mtoto mdogo na kingine ni ubize na masomo nilikuwa nasoma ndiyo maana ukaona kimya ila hata hivyo najiandaa kurudi mapema“Alisema Keisha.

Aligusia pia kwa kudokezea maswala ya kisiasa kama yamemuangusha kwenye muziki Keisha amesema “Siasa haijaniathiri chochote kile kwani mimi siasa naichukulia kama ni jambo la kawaida ambalo linalenga jamii nzima yaani siasa ni maisha ya watu na sio muziki

 

Comments

comments

You may also like ...