Header

Ne-Yo ampongeza Diamond Platnumz

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania Naseeb Abdul a.k.a Diamond Platnumz anayezidi kuzungumziwa zaidi kupitia bidhaa yake mpya ya manukato ya Chibu Perfume apokea pongezi za wazo lake la biashara kutoka kwa msanii wa Kimarekani Ne-Yo.

Akizungumzia jinsi biashara hiyo inavyoendelea tangu kuzinguliwa kwake katikati mwa wiki iliyopita Diamond amesema kuwa wapo wasanii wengi marafiki zake walioonyesha kuguswa kwa wazo lake la kibiashara na kumpa pongezi ambapo Ne-Yo alimtafuta na kumpongeza kwa hatua hiyo ya bidhaa ya Chibu.

Aidha Diamond hakusita kuzungumzia mapokeo na pongezi kutoka kwa watu wake wa karibu Diamond amesema “nje na ndani ya Tanzania ni wengi sana …wengi wamekuwa wakinisupport wengine wakipost kabisa, wengine wanazo akina Kcee na watu wengine sana akina Jah Prayzah rafiki zangu wengi sana hata Ne-Yo amenitumia message pia ameniambia hongera sana thats a big step pia namshukuru sana sana”Alisema Diamond alipokuwa akiongea na Ayo Tv.

Hata hivyo Diamond ametoa shukrani za dhati kwa serikali ya Tanzania kwa ujumla kwa kuthamini wazo lake la biashara hiyo ambalo anaamini kupitia yeye ni wengi watapata ujasiri wa kuthubutu kufanyia kazi mawazo yao kwa lengo la kulijenga taifa lao na maisha yao kwa ujumla.

Comments

comments

You may also like ...