Header

Simon Msuva kutua Uarabuni

Winga wa Yanga na Timu ya Taifa Tanzania,  Simon Msuva, safari ya kuelekea soka la kimataifa huenda ikawa iko tayari sasa, baada ya klabu ya MC Alger ya Algeria kupania kumtoa mitaa ya Jangwani nyota huyo.

Tetesi kutoka mitaa ya Jangwani zinasema kuwa wawakilishi  wa MC Alger wamewasili nchini juzi mchana na kwenda moja kwa moja Uwanja wa Taifa kuangalia mechi ya Kombe la Shirikisho (FA) kati ya Yanga na Tanzania Prisons na Yanga kushinda mabao 3-0 na kutinga nusu fainali huku Msuva aikwa moja ya wafungaji kwenye mchezo huo.

Chanzo chetu kinasema kuwa MC Alger wamekuja kukamilisha mazungumzo ya kumsajili Msuvu baada ya kuvutiwa na uwezo wake katika mechi mbili alizocheza dhidi yao kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika na Yanga kutolewa kwa jumla ya mabao 4-1.

Msuva amebakisha takribani miezi tisa kumaliza mkataba wake Yanga baada ya kuitumikia kwa mafanikio akitokea Moro United katika msimu wa 2013/14.

Comments

comments

You may also like ...