Header

Singida United yamnyatia Ally Mustafa “Barthez”

Klabu ya Singida United ambayo imepanda daraja msimu huu ipo mbioni kuinasa saini ya kipa namba mbili wa Yanga Ally Mustafa, kwa ajili ya msimu ujao wa ligi ya Vodacom Tanzania Bara.

Mwalimu msaidizi wa Timu ya  Singida United Fredi Minziro ameiambia DizzimOnline mazungumzo yao na kipa huyo yamefikia pazuri na kilichobaki ni kusaini mkataba kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo ili aanze kuitumikia msimu ujao.

Ni kweli tulikuwa na mazungumzo na Ally, tunaamini ni kipa mzuri ambaye anaweza kutusaidia msimu ujao na hiyo ni kutokana na uwezo aliokuwa nao licha ya kukosa nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza kwenye timu yake ya Yanga,” amesema Minziro

Alli amepotea machoni kwa Wanajangwani toka pale alipomruhusu Shiza Kichuya kuisawizishia Simba dakika za lala salama kwenye mchezo wa ligi kuu ambao uliisha simba kutoshana nguvu kwa kufungana 1-1.

Comments

comments

You may also like ...