Header

Yanga watoa onyo kali kwa Mbao FC

Siku moja baada ya kupangwa kwa droo ya nusu fainali ya kombe la shirikisho, mabingwa watetezi wa michuano hiyo Yanga wamesema wapo tayari kufunga safari kuelekea jijini Mwanza kuifuata Mbao FC mwishoni mwa juma hili kuikabiri klabu hiyo.

Yanga wamepangwa na Mbao FC ambao watakua nyumbani kwenye uwanja wa CCM Kirumba mwishoni mwa juma hili kwa ajili ya mchezo huo ambao utaamua nani ataingia fainali ya kombe la Azam Sports Federation Cup.

Katibu mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa akiongea mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam amesema wamejiandaa kukabiliana na lolote katika michuano hiyo, na walipoona wameangukia kwa Mbao FC tena katika uwanja wa ugenini waliipokea hatua hiyo kwa mikono miwili na wamejipanga kutekeleza majukumu yao kwa kupata matokeo na kuwaonya wajiandae  vizuri.Tazama video hapa chini Mkwasa akiongea na waandishi wa habari

Comments

comments

You may also like ...