Header

Ben Pol alizwa na mfumo wa elimu nchini

Msanii wa muziki kutoka Tanzania Ben Pol anayetamba na ngoma yake ya ‘Phone’ amesikitishwa na ukosefu wa elimu kwa baadhi ya watoto huku akisema vifo vya  wazazi muda mwingine vinachangia namna moja ama nyingine.

Ben Pol amesema hayo kupitia kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii,kutokana na ripoti nyingi zikiwa zinadai kuwepo kwa changamoto kubwa hususani kwa nchi masikini zenye kipato cha chini.

Inaniumaga sana nikiona vijana wanakosa kupata elimu kwa sababu ya majanga yanayojitokeza katika maisha, sana sana kifo cha mzazi huwa kinachangia sana hii ishu. Najua wengi tumeguswa kwa namna moja au nyingine na hili” Ameandika Ben Pol kwenye ukurasa wa Instagram.

Vile vile msanii huyo ameshauri kutafutwa suluhisho la jambo hilo mapema ili kuweza kuokoa vizazi vya sasa kwa maana ndiyo viongozi wa kesho katika taifa hili.

Comments

comments

You may also like ...