Header

Maisha ya uokovu yamtenganisha Goodluck Gozbert na marafiki zake

Msanii na mtayarishaji wa kizazi kipya cha muziki wa injili kutoka Tanzania anayefanya vizuri na nyimbo kubwa kama ‘Ipo siku’ na ‘Hao hao’ Goodluck Gozbert amewashauri wote ambao tangu ameigia katika maisha ya ukovu wanakosa mchango wake.

Akizungumza na Dizzim Online Goodluck ambaye amekuwa mchango mkubwa katika uandishi na utayarishaji wa muziki wa bongo fleva kama LollyPop amesema kuwa wanaoyumba kwasababu ya kutokuwepo kwake kwenye maisha yao wanahitaji kukubali hali halisi na kutafuta uwezekano wa kuendelea na maisha bila kulalamika kwa nia ya kupiga hatua.

“kama kuna mtu anakuja kwenye miasha yako kwa ajili ya kukusaidia wewe kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine…huyo mtu akiondoka kwenye maisha yako sio wakati wa wewe kuanza kulalamika na kumsubiria arudi ni wakati wa wewe kufanya jitihada zako binafsi kusogea hatua nyingine ambazo mungu amekupa. Kwahiyo kimsingi ni kwamba kama kuna mtu yoyote ambaye labda nimewahi kuwa kwenye maisha yake na sasa sipo anatakiwa kujua kwamba ulikuwa ni wakati na msimu wa mimi kuwepo kwenye maisha yake na msimu huo haupo sasa nipo kwenye maisha mengine kwa hiyo anatakiwa kukubali hiyo na kujua namna ya kupiga hatua nyingine nzuri zaidi na kubwa” Amesema Goodluck Gozbert.

Hata hivyo Goodluck Gozbert ameshiriki kufanikisha kazi kubwa za wasanii Tanzania katika kuandika, kutayarisha ikiwa ni pamoja na Moyo mashine ya Ben Pol na kuandikia wasanii wengine kama Mo Music na Barakah The Prince.

Comments

comments

You may also like ...