Header

Pogba hatarani kuikosa Manchester Derby

MANCHESTER, ENGLAND - DECEMBER 31: Paul Pogba of Manchester United during the Premier League match between Manchester United and Middlesbrough at Old Trafford on December 31, 2016 in Manchester, England. (Photo by James Baylis - AMA/Getty Images)

Kocha wa Manchester United amepata hofu kuwa Paul Pogba anaweza kuikosa mechi ya Alhamisi dhidi ya Manchester City maarufu kama Manchester Derby baada ya kupata majeraha dhidi ya Burnley wikiendi iliyopita.

Mourinho alisema kuwa hajui kama Pogba aliumia au alikuwa amechoka, lakini kocha huyo wa Mashetani Wekundu amesema kuna uwezekano mkubwa nyota huyo akaikosa mechi ya Alhamisi katika uwanja wa Etihad.

Sijui kama ameumia au ni uchovu wa misuli tu, sijui kwa kweli. Lakini kama hataweza kucheza Alhamisi, basi hatacheza. Tutachezesha mchezaji mwingine na hatuna sababu ya kulia,” Mourinho, ambaye tayari amewakosa Chris Smalling, Phil Jones, Marcos Rojo, Juan Mata na Zlatan Ibrahimovic, aliwaambia waandishi.

Pogba alilazimika kutoka dakika za mwisho baada ya timu yake kushinda 2-0 katika uwanja wa Turf Moor Ligi Kuu Uingereza baada ya kuonekana akiugulia maumivu

Comments

comments

You may also like ...