Header

Simba wagwaya kuzungumzia ‘Pointi tatu’ za mezani

Klabu ya Simba imetangaza kuahirishwa kwa mkutano wa viongozi wa klabu hiyo na waandishi wa habari,Hii ikiwa ni siku ya pili baada ya Kamati ya Sheria, Haki na Hadhi za Wachezaji kutengua maamuzi ya Kamati ya Saa 72 yaliyoipa pointi tatu na mabao matatu katika malalamiko yao dhidi ya Kagera Sugar.

Taatifa rasmi kutoka Msimbazi imesema kikao hicho kimeahirishwa na waandishi watataarifiwa muda na mahali wa kikao kingine kitakapotangazwa.

Kwa sasa Simba imepiga kambi mjini Morogoro kujiandaa na mchezo wake wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Azam utakaopigwa siku ya Jumamosi.

Comments

comments

You may also like ...