Header

Timmy T Dat afichua siri ya kufanya kolabo tena na Sudi Boy

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Kenya kutoka katika record lebo ya Kaka Empire, anayefanya vizuri na ngoma yake mpya na Sudi Boy ‘Zile mbili’ Timmy T Dat atoa sababu za kwanini  amerudi tena kufanya kazi na msanii Sudi Boy mbali na kuwa walisha fanya kazi kabla ya wimbo wao mpya..

Akizungumza na Dizzim Online Timmy amesema kuwa sababu za kuonekana tena kufanya kazi ya pamoja na Sudi Boy ni dalili za kuwa kuna furaha ya kikazi linapokuja suala la wawili hao kufanya kazi za pamoja.

“mimi na Sudi Boy ni marafiki na kilichotokea ni tumeendana sana, baada ya sisi kufanya kazi iliyopita tulijiuliza mbona isiwezekane tena katika kazi nyingine ndo tukafanya na kama mlivyoona kazi imetoka nzuri na vile fans wameipokea ni kuonyesha wanapenda tukifanya kazi pamoja” Alisema Timmy T Dat.

Hata hivyo Timmy T Dat ameongeza kwa kusema kuwa anamini ngoma ya ‘Iromo’ aliyofanya awali na Sudi Boy ni ngoma kali na mashabiki walionesha kila dalili za kuwakubali katika ngoma ile hivyo ujio huu tena mpya wa kazi yao ya ‘Zile mbili’ itakata kiu ya wote ambao bado wanependa muuganiko wao wa kikazi.

Comments

comments

You may also like ...